GET /api/v0.1/hansard/entries/1224702/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1224702,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224702/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": ". Marekani inakuja kusema kuwa ni demokrasia wanaume kupandana kama mbuzi ama wanawake kupandana. Hiyo sio demokrasia ila ni ushetani. Viongozi msiogope. Nimewaambia kuwa mkitaka mchukue viza yangu. Viza tunayotafuta duniani ni viza ya ufalme wa mbinguni. Tusiogope hivi vijikaratasi vidogo na sheria zao. Wazungu walikuja hapa Afrika wakatutoa katika utamaduni wetu, wakatudhulumu, wakatufanya wakimbizi wa ndani kwa ndani na kuwaua wazee wetu. Wakawanyanganya ardhi na kuwatesa hata na kuwafanya maabusu na kuwauza kama mifugo katika mataifa ya nje ili Waafrika waende wafanye kazi chafu chafu. Leo, hata mfano ukitokewa katika sinema na vitabu, huwa wanaonyesha kuwa watu weupe ni malaika na watu weusi ni mashetani. Jamani fungueni macho nyinyi Waafrika! Alama ya shetani ni nyeusi. Hakuna siku utaona shetani mweupe. Hata katika sinema, mwizi, muuaji, mbakaji na mtu mbaya ni Mwafrika. Hawawezi weka mwizi au shetani mzungu kwa sababu wamedharau hata ngozi yetu. Ukienda saa hii kule kwao, wanabagua Waafrika. Mnaitwa monkeys, gorilla na kila aina ya majina na mnacheka mkisema wazungu. Eti mzungu akitoa hewa ni marashi na Mwafrika akitoa hewa ni uchafu. Amkeni kumekucha! Mkatae haya ya wazungu na mwaite kwa majina yao. Mimi leo namtaja Balozi wa Marekani ambaye wiki iliyopita alifanya mikutano na mashoga na wasagaji na akasema katika lugha ya Kimombo kuwa ni Democracy and HumanRights. Hakuna haki za binadamu pale. Muende mfanye usagaji huko kwenyu. Chukueni hao mashoga na mwapatie viza, greencard na hizo haki za binadamu katika mataifa yenyu. Nchi hii ya Marekani imeharibu dunia nzima na milki za Kiarabu kwa vita za mafuta. Imeharibu mataifa mengine kwa sababu ya madini. Imeharibu kila nchi Afrika."
}