GET /api/v0.1/hansard/entries/1224710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1224710,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224710/?format=api",
"text_counter": 94,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "mashoga wa Marekani. Amezungumzia swala linalotuhusu sisi Wakenya. Kwa hivyo, kwa sababu ya kidiplomasia na heshima ya mataifa, tutaheshimiana lakini ukienda kinyume na Katiba ya nchi yetu, hatutaheshimiana. Kwa hivyo Mhe. Spika wa Muda, sijamtaja kwa njia mbaya ila nimemtaja kwa sababu yeye anajaribu kufanya mambo kinyume na Katiba ya nchi. Sisi tunaheshimu Katiba yao na wao pia waheshimu Katiba yetu, dini na utamaduni zetu kama Wakenya na Waafrika. Mhe. Spika wa Muda, naona muda unanipa kisogo na Wabunge wenzangu wanataka kuchangia. Nitamwachia dada yangu dakika zilizosalia ili aweze kuchangia lakini ningeomba uwape muda kidogo wangwana hawa ili waweze kuzungumzia haya maswala. Naomba Bunge hili lipitishe Hoja hii tukisubiri Mswada wa Mhe. Kaluma. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Langu la mwisho ni kuwaomba Wabunge waweze kupasisha Hoja hii na kuhakikisha kwamba hizi tabia hazikaribii watoto wetu na kizazi kijacho. Wahakikishe kwamba hakuna uchapishaji wa taarifa zinazokuza mahusiano ya jinsia moja, na uonyeshaji wa uchafu wa wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake katika vipindi vya runinga. Haya yote yanafaa kuzuiliwa na Serikali ya Kenya ili tulinde kizazi kijacho. Nawasilisha Hoja na kuomba Wabunge waweze kupitisha Hoja hii tunaposubiri Mswada wa Mhe. Kaluma ambayo itapelekwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Kenya aitie kidole ili tusahau haya mambo mara moja tulinde vizazi vyetu. Asanteni sana na Mungu awabariki."
}