GET /api/v0.1/hansard/entries/1224786/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1224786,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1224786/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Lillian Siyoi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Bw. Spika wa Muda. Kama mkaazi wa Trans Nzoia, wakati mmoja niliomba kuunganishiwa umeme. Niliambiwa kuwa transforma zinaweza tu kupeanwa kwa nyumba kadhaa. Nilipewa bajeti ya Ksh1.8 milioni. Swali langu kwa Shirika lile lilikuwa: je, transforma hii ingekuwa yangu binafsi au vipi? Nilipata shida sana. Mambo haya ya ukiritimba yamekuwa magumu kwa sababu hakuna pahali pengine pakukimbilia ili kupata umeme. Ni vyema kama tutakubalia pia KenGen isambaze umeme. Tunaona kuwa KenGen wanauzia KPLC umeme kwa bei nafuu na mwishowe KPLC hutuuzia umeme huo huo kwa bei ya juu zaidi. Naomba pia turuhusu KenGen isambaze umeme kwa wananchi."
}