GET /api/v0.1/hansard/entries/1225032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1225032,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1225032/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, ni Sen. Cherarkey ndiye ananichanganya. Mimi ninaunga mkono dua hii kwamba maslahi ya wauguzi yanapaswa kuangaliwa. Wakati wa homa kali ya COVID-19, wauguzi wengi waliajiriwa na kupewa mkataba. Baada ya COVID-19, hakuna jambo lolote ambalo wanaonekana kufanya kulingana na wale waliowaajiri. Wameleta malalamishi yao hapa ili tuyaangalie. Langu ni kuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Afya waangalie haya mambo kwa undani. Tusianze kuyapapasa haya mambo kwa sababu hili ni donda sugu. Ni masuala nyeti ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa kina. Wapo madaktari wengi katika kaunti zetu ambao hawana kazi. Wengine tayari wamepewa nambari ya kuajiriwa na Serikali kwa hiyo hawawezi kutafuta kazi mahali pengine. Ni vizuri Kamati husika ishughulikie mambo haya. Ni wengi ambao wanazidi kujiunga na hii wizara hii ilihali wale walioko, hawalipwi."
}