GET /api/v0.1/hansard/entries/1225048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1225048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1225048/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13733,
"legal_name": "Agnes Kavindu Muthama",
"slug": "agnes-kavindu-muthama"
},
"content": "Bw. Spika, ninashukuru kwa nafasi hii ili nichangie suala ambalo Sen. Cherarkey amelileta hapa Bungeni. Madaktari wanafanya kazi ngumu sana. Usiku sisi tukiwa usingizini, wao wanahudumia wagonjwa hospitalini. Ni muhimu kuwa maslahi yao yangaliwe kwa kina. Kwa hivyo, Wizara ya Afya haistahili kupinga hizi pesa ambazo madaktari wanastahili kupatiwa baada ya uamuzi wa Bunge. Ni lazima watoe hizo pesa ili ziende mashinani kuhudumia madaktari wetu. Hakuna watu ambao hufanya kazi ngumu kama madaktari. Hata mtu akiwa katika hali mahututi, daktari atamhudumia mpaka atoke hospitalini akiwa mzima na katika hali ya kujisaidia. Hatutaki madaktari wetu wagome kwa sababu ndio wapate pesa wanazostahili. Hata makaazi yao ni duni kabisa. Ninaomba serikali za kaunti zichunguze nyumba wanamoishi hao madaktari. Madaktari wanastahili kuwa na Amani. Wanastahili kuwa wenye furaha wanapotoka nyumbani kuelekea kazini ili waweze kuhudumia wagonjwa inavyostahili. Ninaunga mkono Ardhilhali ya Sen. Cherarkey."
}