GET /api/v0.1/hansard/entries/1225576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1225576,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1225576/?format=api",
"text_counter": 662,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ngoja ninakuja. Usifanye haraka, mosmos. Chama cha Muungano wa Azimio la Umoja kilipeana taarifa kwa mkuu wa polisi wa kituo cha Nairobi, kuarifu kuhusu maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike katika Wilaya ya Jiji la Nairobi, tarehe 20.03.2023. Walitumia haki yao kulingana na Kipengele 37 cha Katiba kuandamana kwa amani bila kubeba silaha zozote. Siku ya maandamano ilikuwa siku ya amani sana. Mimi mwenyewe nikiwa mmoja wa wale watu, tuliweza kutoka hapa kama waheshimiwa na tukaenda tukisema ya kwamba ni haki yetu kulingana na kipengele cha 87 ya kwamba tunaweza kuandamana. Ni jambo la kushangaza. Na mimi naomba, isije ikatokea upande wowote kwa sababu, umeamka usiku wa leo ukiwa upande huu, kesho, unaweza amka ukiwa upande ule mwingine. Hio ndio hali ya maisha na hali ya vile watu wanaishi."
}