GET /api/v0.1/hansard/entries/1226704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1226704,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226704/?format=api",
    "text_counter": 503,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Shukran sana, Mhe. Spika wa Muda. Nimeona hisia tofauti tofauti kutoka kwa Wabunge lakini nataka kwanza kuzungumzia kijana aliyeuawa. Tangu nizaliwe – na nina umri wa miaka 41 – katika taifa hili, ni mtu mmoja peke yake ambaye huitisha maandamano. Maandamano hayo huwa si ya amani. Katika kila maandamano, lazima mtoto wa watu afe. Hawa watu wanaoitisha maandamano ni wale wale waliofanya zile salamu za cheque . Walisalimiana, wakapeana pesa, wakapandisha bei ya unga hadi Ksh230. Sasa wanakuja kutufunza sisi jinsi ambavyo tutaendesha nchi hii. Ni lazima Raila Odinga aambiwe ukweli kinagaubaga. Waswahili wanasema, “Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji.” Raila The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}