GET /api/v0.1/hansard/entries/1226709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1226709,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226709/?format=api",
"text_counter": 508,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": " Shukran sana Mhe. Spika wa Muda. Unajua kuna watu ambao mungu wao akitajwa hawatulii. Lakini yale nataka kusema ni kwamba Rais William Ruto ameshika usukani wa nchi hii hivi majuzi. Imekuwa miezi sita. Hata na mimba, mtoto hawezi akazaliwa kwa muda wa miezi miwili. Ni lazima tupatie Rais aliye mamlakani nafasi ya kuongoza nchi hii. Nchi hii imeharibiwa na wale wale wanaoitisha maandamano. Juzi tumepoteza pesa katika taifa hili. Watoto wameuawa kule Kisumu. Ajabu ni kwamba katika Kenya nzima, ni sehemu mbili tu zilizofanya maandamano. Mbona Mombasa, Central, North Eastern, na Western hawana shida? Ni kwa nini lazima iwe ni Kisumu, Kibera, na hapa Embakasi? Tumechoka kama viongozi. Ni lazima Kenya iendeshwe katika njia ya haki na ya kikatiba. Hatutakubali muungano haramu wa kusumbua wananchi kila siku. Biashara zimesimama na watu hawawezi kutembea kwa amani. Angalia Afrika Kusini: waliomba wafanye maandamano. Jifunzeni kutoka kwa wale badala ya kuingia barabarani na kupora mali ya watu, kupiga na kuumiza watu, halafu mnakuja kusema kuwa mtatuongezea maandamano yawe kila Jumatatu na Alhamisi. Nchi hii iko na Serikali, Wakenya, na sheria. Fahamu kuwa hiyo sheria ni lazima ifuatwe. Hatutakubali! Sikizeni tena vizuri."
}