GET /api/v0.1/hansard/entries/1226794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1226794,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226794/?format=api",
    "text_counter": 593,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hatimaye kuchangia Hoja hii. Ni jambo la aibu sana kwamba miaka nenda miaka rudi, mambo ni yale yale ya maandamano. Wahusika ni wale wale. Tunamjua mhusika mkuu anayeitisha maandamano miaka nenda, miaka rudi. Watoto wa watu wanamwaga damu na kufa kwa maandamano. Wanaleta vijisababu ili wapate handshake ama nusu mkate. Wakipata hiyo, wanakula peke yao. Hawagawanyi ule mkate wale pamoja na watu ambao wanaenda kwenye maandamano na zile familia za wale watu wamepoteza wapendwa wao. Mhe. Spika wa Muda, ni vizuri kulalamika kama kuna kosa lakini kuna njia ya ustaarabu ambayo tunaweza kuleta hoja zetu. Tumeona watu wakifanya hivyo lakini si haya mambo ambayo tunajionea katika Kenya yetu ya watu kwenda barabarani, kuharibu mali ya watu na hatimaye watoto wa watu wanapoteza maisha. Hadi lini kina mama wataendelea kulia kwa ajili ya watoto wao? Itafika mahali tutawaambia wale miili ya wale watu ambao wanafariki. Haifai na wala haistahili! Tunayalaani hayo maandamano kwa sababu si ya amani kama wanavyosema. Ni lazima tuheshimiane na tumpatie Rais aliye mamlakani nafasi ya kufanya kazi. Hata mama akishika ujauzito, inachukua miezi tisa kuweza kujifungua na kupata mtoto. Hakuna mimba inazaliwa katika muda wa miezi mitatu au minne. Kwa hivyo, tumpatie Rais William Samoei Ruto nafasi ya kufanyia watu kazi. Watu wanaogopa kwa sababu wanajua Rais William Samoei Ruto ni mchapa kazi. Ndiyo maana wanaona wakimpatia nafasi, atawaibisha. Ndiyo maana wanataka kwenda barabarani."
}