GET /api/v0.1/hansard/entries/1226808/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1226808,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226808/?format=api",
    "text_counter": 607,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Yangu hayatakuwa mengi ila ningependa niseme kwamba ni jambo la kustaajabisha wakati nchi zingine zina shughulika na mambo ya kujijenga, nchi yetu ambayo imemaliza uchaguzi hivi majuzi inang’ang’na na mambo ya kupigana. Sisi tumemaliza uchaguzi juzi na kila Mheshimiwa aliye hapa hawezi kubali kuambiwa arudie uchaguzi. Kwa nini tulikubali matokeo wakati tulitangazwa kuwa washindi ilhali tunakataa kukubali ushindi wa wengine? Mimi siungi mkono hii hali ambayo inaendelea. Maafa ambayo yametokea Kenya hii tangu uhuru ni mengi sana. Hao watu walikufa wakipigania haki zetu au waliuawa na Serikali zilizokuwa wakati huo. Haistahili wakati huu ambapo kuna demokrasia katika nchi ya Kenya kuona maafa ambayo yanatendeka kwa sasa."
}