GET /api/v0.1/hansard/entries/1226809/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1226809,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226809/?format=api",
    "text_counter": 608,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
    "speaker": null,
    "content": "Nawaomba rafiki zangu kwamba tuvumilie hii Serikali ambayo bado ni changa ifanye kazi. Ningependa kila mtu, akiwemo Mhe. Salasya, ayasikie haya. Wengine wetu tulifungwa na kuyapitia mabaya, lakini tukaamua tuvumilie na tuipe hii Serikali muda wa kufanya kazi. Watu wengine wakiwaona askari-polisi wanakimbia kujificha ndani ya choo kisha watuambia eti wanataka demokrasia. Sisi tunajua uovu ambao Serikali iliyopita ilitenda. Tunafahamu wizi ambao ulitendeka. Tunakumbuka jinsi ambavyo Shilingi za Kenya bilioni 16 ziliibwa kwa usiku mmoja, kwa chini ya dakika ishirini na sita. Wengine waliiba Shilingi za Kenya bilioni 90. Haya maandamano hayaendelei eti kwa sababu Wakenya wako hali njaa ila ni kwa sababu wanataka kuficha yale maovu ambayo yalitendeka kwa Serikali iliyopita."
}