GET /api/v0.1/hansard/entries/1226810/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1226810,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226810/?format=api",
"text_counter": 609,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
"speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
"speaker": null,
"content": "Sisi tuna uchungu ila tunavumilia na kunyamaza tu. Ni muhimu watu wafahamu hata na sisi tuliumia sana ila hatukuuliza chochote. Tumesema Serikali ipewe muda wa kufanya kazi. Kwa hivyo, watu ambao wanauawa kwenye maandamano ni wale ambao wemelipwa kuzusha vurugu. Mlikuwa kwenye Serikali ya Handshake, mkatawala kwa muda wa miaka mitano ila mlishindwa kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo nchini. Mpe aliyeshinda uchaguzi nafasi afanye kazi kwa muda huu wa miaka mitano ijayo kisha mje kuuliza kama aliimarisha uchumi au la. Ningependa kumwuliza Rais Mstaafu aende kupumzika maana alikuwa na miaka yake kumi ya uongozi ambayo hakusumbuliwa. Awache kusumbua na kutisha raia wa Kenya. Kuna maswali mengi ambayo tungependa kumwuliza ila tumewacha maana hatutaki kukumbuka yaliyopita. Enda nyumbani ukale starehe zako na uwachane na Wakenya wafanye maendeleo yao."
}