GET /api/v0.1/hansard/entries/1226946/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1226946,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226946/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Naibu Spika asanti kwa kunipa hii nafasi ili nichangie hii mada ya kuwakaribisha wanafunzi wa shule ya upili ya Lenana. Nimesikia ndugu yangu Sen. M. Kajwang’ amesema kuhusu shule za upili ilhali sikua na bahati ya kusomea katika shule hii lakini nilisoma na ndugu yake Joe Okoto Kajwang’ katika shule ya upili ya Kisii. Baadaye tulikuja kupatana katika chuo kikuu cha Nairobi na pale ndipo nikapatana na ndugu Sen. M. Kajwang. Ingawa tulihudhuria zile shule ambazo hazipatikani katika runinga tulijaribu sana na kufika hadi mahali tupo. Jambo la pili ningetaka kumwambia Sen. M. Kajwang’ na wanafunzi ni kuwa nimezungumza katika lugha ya Kiswahili kwa sababu ningependa kuwasihi nyinyi vijana wadogo kuwa lugha ya taifa ni muhimu. Popote ambapo utakapotembea nchini Kenya au ulimwenguni ukiulizwa umetoka wapi na kusema Kenya; jambo la kwanza anauliza ni habari gani. Ningependa kuwasihi wanafunzi wa shule ya upili ya Lenana kwamba shule yenu inalo jina nzuri, ina heshima na kuna viongozi wengi waliosoma katika shule hii. Tafadhali muwe na heshima, nidhamu na muendelee kufanya vizuri. Baba zenu hawana utajri mwingi. Akili unazotoa kwa masomo ndio itakupa nafasi ya kutembea ulimwengu. Nadhani mnanielewa. Ikiwezekana zingatia yale mawaidha tunayotumia katika hili Bunge ama Standing"
}