GET /api/v0.1/hansard/entries/1226993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1226993,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1226993/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "kushangaza sana. Kuna wafanyikazi wengi katika shule za wanafunzi wanaoishi na ulemavu ambao hawajalipwa mishahara kwa miezi tisa au zaidi. Bw. Naibu Spika, shule za wanaoishi na ulemavu zinahitaji walimu. Kando na walimu, wale wanaohitajika ni caregivers ama watu watakaoangalia wale watoto. Wengine wanahitaji kuoshwa, kusukumwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Tutaangalia hii Taarifa kwa undani. Naomba Kamati ya Labour and Social Welfare iangalie pia. Katika Bunge la Kumi na Mbili, tulisukuma sana Wizara ya Leba ipate takwimu za kutosha na kuandikisha wale wote wanaishi na ulemavu na pia kuhakikisha wameenda shuleni. Nashukuru Sen. Crystal Asige na anafanya kazi nzuri ya kupigania wale wanaoishi na ulemavu Kenya. Tutangojea hiyo ripoti itakayokuja kutoka kwa hio Kamati na najua mambo ya walemavu yatazidi. Lakini kwa sasa, tupate takwimu au data ya kutosha kutoka kila kaunti ya wale wanaoishi na ulemavu. Zile pesa wanahitaji kupata kama kwa Inua Jamii, wote waweze kupata."
}