GET /api/v0.1/hansard/entries/1227256/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1227256,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1227256/?format=api",
    "text_counter": 408,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Mimi kama Seneta wa Bungoma, hatutakubali kubinafsisha Kiwanda cha Sukari cha Nzoia pasipo kuhusisha wapigakura wa Kaunti ya Bungoma na watu wengine ambao wanatoka pembe mbali mbali za Kenya. Ni lazima Mawaziri waje hapa ili tuwaweke kwa msasa na ikiwezekana tuwatundike juu ya msalaba jinsi Sen. Mungatana alivyosema. Wakenya wana haki ya kupata majibu kutoka kwa Mawaziri. Kuna masuala ya mipaka hapa Kenya. Kumekuwa na shida ya barabara kule Malaba na Busia. Jinsi nilivyosema jana, kazi ya Mawaziri si kupiga picha. Wanafaa kuja kutueleza kwa sababu tunawapa bajeti. Tunafaa kujua kama tunapata haki kama Wakenya ama kazi yao ni kujinufaisha na kufurahia matunda ya Serikali."
}