GET /api/v0.1/hansard/entries/1227257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1227257,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1227257/?format=api",
"text_counter": 409,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Naunga mkono Kiongozi wa Wengi kwamba Mawaziri wawe wakija. Hata hivyo, jinsi Sen. Sifuna alivyosema, tunafaa kufungua milango na kuzungumza Wakenya wakisikia. Kama ni lugha tuseme na kama ni mifano tutoe kwa sababu wanaporudi kwa Baraza la Mawaziri, wanafaa kwenda kumwambia Mhe. Rais kwamba tumewauliza maswali na wameshindwa kujibu ili awape nafasi ya kwenda kufanya masomo ya ziada nyumbani ili tukiwaita tena watupe majibu tunayotaka."
}