GET /api/v0.1/hansard/entries/1227413/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1227413,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1227413/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono Hoja iliyotolewa na Sen. Osotsi. Baadhi ya wanafunzi katika shule za upili, vyuo vikuu na vyuo anuwai, wako nyumbani kwa sababu hawana karo. Serikali za kaunti zimeweka wanafunzi hawa katika mfumo wa kuimarisha masomo yao kwa wale ambao ni wachochole kifedha. Hivi kwamba, serikali ya Kitaifa imekosa kuwachilia pesa kuenda mashinani huku tukizingatia kwamba sisi kama Seneti na Bunge la Kitaifa tulitia sahihi na kupitisha kwamba pesa ziteremuke. Hivi kwamba, ninaunga mkono mapendekezo ya Seneta Osotsi kwamba tuelezwe ni kwa nini kunakucheleweshwa kwa fedha za kuenda kwenye kaunti ilhali tunaona Mawaziri humu Kenya wakizuru nchi mbali wakipiga picha na video. Ilhali wananchi wanapiga miayo na kusaga meno."
}