GET /api/v0.1/hansard/entries/1227516/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1227516,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1227516/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa nafasi kuwakaribisha wanafunzi wa kutoka Kimugumo Girls. Shule hii iko Gichugu. Hiyo shule iko mahali ambapo Gavana wa Kirinyaga Mheshimiwa Ann Waiguru ametoka. Ningesema ya kwamba mnapotia bidii na fora katika masomo yenu, mko na watu walioko mbele yenu wanawowanyesha kuwa masomo ni muhimu. Mkiweka bidii, mtaenda mbali sana. Mimi shule niliyosomea, mimi ndiye nilikuwa mwanafunzi pekee. Sikuwa na nafasi ya kwenda shule kama Lenana School au shule iliyo na wanafunzi wengi. Shule yetu ilikuwa na mwalimu mmoja. Hivyo basi, hiyo ni historia ambayo nitapeana siku nyingine. Kuwa mwalimu mmoja, ukiwa mwanafunzi mmoja na unaanzia huko peke yako, ilinibidi nitunge sheria pamoja na mwalimu. Hiyo pia inasaidia mahali yake. Nawakaribisha wanafunzi. Najua tukimaliza hapa tutaonana pale nje. Tuna desturi yetu ya watu wa Kirinyaga. Nawashukuru na kuwakaribisha siku ya leo. Mtasoma mengi. Asanteni sana."
}