GET /api/v0.1/hansard/entries/1228271/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1228271,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1228271/?format=api",
"text_counter": 57,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Naibu Spika, kwa kuonyesha usawa kwa wote. Ninataka kuungana na wewe kuleta risala za rambirambi za watu wote wa Kaunti ya Laikipia na kuzipeleka kwa watu wa Banisa kwa kupoteza kiongozi Mheshimiwa Kulow Hassan ambaye tunamfahamu. Alijitolea kufanyia wananchi kazi bila kupendelea upande wowote kama ulivyofanya. Ninaleta pia risala kutoka familia yangu. Ndugu zetu wanaopeleka bodaboda wanafaa kuwa waangalifu kwa sababu ajali hizi zinatokea kwa watu wengi. Huyu ni mmoja wetu tunayeletea risala za rambirambi lakini kila siku, watu wetu wanapata ajali hizi na wengi wanakufa. Pia vijana wa bodaboda wanapata maafa. Wagonjwa wengi katika hospitali zetu ni kwa sababu ya majeraha waliyopata katika ajali za bodaboda. Siku hii ni ya huzuni kwa kuwa tumempoteza kiongozi ambaye tulienzi na sasa tutamkosa. Tunwashukuru watu wa Banisa kwa kumchagua mara ya pili kwa sababu yeye alikuwa mchapa kazi. Bw. Naibu Spika, ninaungana na wewe kuwakaribisha ndugu zetu kutoka Uganda. Ukitembea Kampala, utawapata wakiongea kwa lugha ya Kiswahili. Wanafahamu lugha hii. Kwa hivyo, tunasema Kiswahili kitukuzwe."
}