GET /api/v0.1/hansard/entries/1228357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1228357,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1228357/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika Wa Muda, ninasimama kuunga mkono taarifa hii. Elimu ya uraia ni muhimu sana katika gatuzi zetu. Kama vile inavyosemwa, ujuzi ni nguvu. Wakati mwingi, raia wanaenda kupewa masomo wakati wa kuna uchaguzi. Hata hivyo, maisha hayaanzi na kuisha na uchaguzi. Kuna mambo mengi sana ambayo yanapaswa kufunzwa. Wakati huu, watu wanazungumzia sana jinsi gharama ya maisha imepanda. Tukienda kufunza wananchi kuhusu njia bora za ukulima; mbegu au mimea ambayo wanapaswa kupanda na wakati upi, hii ni elimu muhimu ambayo itafaa katika gatuzi zetu. Bw. Spika Wa Muda, Sen. Murgor amedokezea kwamba shida nyingi zinatokana na wanachi kutoelewa na kukosa ufahamu. Hata wakati ambapo tunapaswa kupanda, hatujui ni mbolea gani ambayo tunatakiwa kutumia. Wananchi wanatumia tu kile ambacho ni cha bei rahisi. Hilo ndilo la muhimu kwao. Ni kwa sababu ya kutokuwa na ujuzi na ufahamu wa maneno. Bw. Naibu Spika, tuizingatie Taarifa iliyoletwa. Tuiwekee maanani, ndiposa wananchi wetu waweze kufahamu na kuelewa. Kama ilivyosemwa, wale wanaofanya maandamano wanawaahidi watu mambo mengi. Lakini, tutapunguza gharama ya maisha kwa kuwambia wananchi ukweli ya kwamba, mambo yanayotendeka katika ulimwengu yanatuathiri hata sisi. Vita vilivyoko nchi ya Ukraine vinatuathiri hapa Kenya. Ni vizuri tuwambie Wakenya ukweli kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta. Ukiangalia, hali ya hewa imebadilika pia. Viongozi wengi wanachukuaa fursa kwa sababu wananchi wetu hawaelewi. Badala ya kuwafunza, wanawaongoza katika njia zisizo kuwa za amani na kufanya maandamano ambayo hayatakuwa na manufaa kwao. Ni vizuri tuwambie watu wakati kama huu wanapaswa kupanda. Hii ni kwa sababu sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya zimenyesha. Tungekuwa tunaongea vile wanaichi wetu watapata mbolea. Na hiyo mbolea isipelekwe mijini kwa sababu watu walio mijini hawapandi. Tunataka mbole hiyo ipelekwe mashambani. Kwa mfano, mbolea isifikishwe tu Nyahururu, bali ipelekwe Marmanet, Rumuruti, Muhoteti, Kinamba, Matanya na Raburia. Taarifa hii inamaanisha"
}