GET /api/v0.1/hansard/entries/1228585/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1228585,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1228585/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bwana Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ardhilhali iliyoletwa katika Bunge hili na Seneta wa Kaunti ya Nandi, Sen. Cherarkey. Masaibu yaliyokumba familia ya mwendazake Mhe. Seroney ni ya kusikitisha katika nchi yetu ya Kenya kwa sasa. Hii ni nchi ambayo ina sheria na mwongozo, lakini hatuwaangalii viongozi ambao wamepita katika kuhudumia nchi yetu kwa siku za nyuma. Ningependa kuwakumbusha katika Bunge hili na lililopita tuliupitisha Mswada wa kulipa kiinua mgongo madiwani waliokuwa wamehudumia katika baraza za miji na manispaa ya zamani kabla ya kuja katika ugatuzi lakini hadi sasa imekuwa hadithi ya nenda rudi. Tutaweka pesa mwaka ujao na utakaofuata lakini mpaka sasa hawajalipwa chochote. Wengi wao wanazidi kufa katika hali ya uchochole kabisa. Masaibu yanayokumba familia ya mwendazake Mhe. Seroney ni mambo ya kusikitisha. Haya yanaonyesha kwamba uhuru uliopiganiwa bado hujakamilika kabisa. Ikiwa kiongozi wa Bunge hili la zamani anaweza kudhalilishwa akiwa hai na pia akiondoka familia yake bado inadhalilishwa. Ina maana hajutapata uhuru kamili katika nchi yetu ya Kenya. Ningependa kumpa moyo Sen. Cherarkey kwamba ameyapitia masaibu fulani lakini kwa siku hizi karibuni amekuwa anajipiga kifua na kusema yuko katika serikali. Lakini ninataka kuwakumbusha kuwa mara nyingine Serikali hula watu wake. Kwa hivyo, fuata nyayo za hayati Seroney. Yeye alikuwa wakili na alihudumu katika Bunge hili kama wewe. Alikuwa kiongozi katika Bunge hili akiwakilisha watu wa Nandi kama wewe. Kwa hivyo, tafadhali Sen. Cherarkey, angalia njia ambayo utakumbukwa kwa mambo mazuri lakini sio kwa kejeli unazofanya katika Bunge hili."
}