GET /api/v0.1/hansard/entries/1228594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1228594,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1228594/?format=api",
"text_counter": 83,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono dua mbili ambazo zimesomwa katika Bunge hili. Ninamshukuru Bw. Waikwa kwa kuleta dua kuhusu shamba lililoko Kambi Simba katika eneo la Rumuruti. Shamba hilo ni zaidi ya ekari 370. Mzee Kenga wa Mwendia alipatia Idara ya Misitu shamba lake mahali panaitwa Lariak. Baada ya kupatiana Lariak, aliaambiwa atabadilishiwa na shamba lingine huko Rumuruti, Kambi Simba. Baada ya kupeana shamba hilo, Serikali haikubadilisha na kutamka ya kwamba shamba hilo sasa ni la Bw. Kenga wa Mwendia. Kwa hivyo, imekuwa vigumu sana kwa watu walionunua shamba hilo kutoka kwa Kenga wa Mwendia, kutengenezewa barabara na Serikali yetu ya Kaunti. Hii ni kwa sababu inasemekana ni shamba la msitu. Inajulikana wazi ya kwamba huwezi kujenga barabara, shule, hospitali ama zahanati katika sehemu hiyo. Hivyo basi, ninaomba Kamati itakayoshughulikia jambo hilo --- Hivi tunapozungumza, ni zaidi ya miaka 43 baada ya lile jambo kutendeka. Bado wakaazi wa sehemu ile wanaendelea kusosoneka. Hakuna barabara, hospitali wala shule. Kwa hivyo, Bw. Waikwa angependa sisi kama Kamati ya Seneti tushughulikie jambo hili ili watu wanaoishi hapo kwetu Laikipia wasiendelee kuteseka. Serikali ilipata shamba iliyotaka pale Lariak lakini haikufanya juhudi shamba lirudi kwa Bw. Mwendia na aweze kushughulikia kadri tunavyotaka."
}