GET /api/v0.1/hansard/entries/1228596/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1228596,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1228596/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Hayo ndio maombi yetu. Ninaomba Kamati itakayoshughulikia jambo hili ifanye halahala ili wakaazi wa Kambi Simba na sehemu zilizoko hapo, waache kusononeka. Bw. Spika, dua la pili la Sen. Cherarkey ni kumhusu Mhe. Seroney. Nimesikiza na kusoma historia kidogo kumhusu Mhe. Seroney. Vile ambavyo ninamjua Sen. Cherarkey na vile nimesoma kumhusu Mhe. Seroney, nimejua ya kwamba tunda halianguki mbali na mti lililotoka. Ushujaa wake na vile anavyoongea bila kuogopa, hilo ndilo jambo. Hata hivi majuzi nilikuwa na woga wakati Sen. Cherarkey alivyonaswa na kutiwa ndani. Nilidhani mambo yameanza kuwa magumu kwake. Kwa sababu Mhe. Seroney alifanya kazi nzuri katika Serikali yetu, tungependa kuomba Serikali iwafidie familia yake. Kulingana na hilo dua, wanaonekana tayari mali yao yote ilinadiwa na wanaishi kwa hali ya ufukura. Baada ya fidia, tuangalie Mhe. Seroney atakumbukwa vipi kwa sababu alitendea Serikali yetu kazi. Alifanya vile alivyopaswa. Kama vile Sen. Kathuri alivyosema, anapoketi katika kiti hicho, anafanya kadiri ya Kanuni za Kudumu za Bunge. Hafanyi jambo lolote akitaka kujinufaisha yeye mwenyewe. Hivyo basi, tungetaka Mhe. Seroney na familia yake watunzwe. Sen. Cherarkey, kwa sababu ya ushujaa huo, alishikwa na kufungwa ijapokuwa haijulikani. Nimesikia Senior Counsel akisema Sen. Cherarkey alishikwa na Serikali na kufungwa. Vile vile, Seneta wa Kaunti ya Mombasa amesema kwamba Serikali hula watoto wake. Lakini ukiangalia Serikali iliyokuwepo, mtu alikuwa anashikwa Ijumaa na kukaa ndani siku tatu. Kiongozi wa Walio Wachache alishikwa kwa masaa matatu. Kwa hivyo, angalau sasa."
}