GET /api/v0.1/hansard/entries/1229023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229023,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229023/?format=api",
    "text_counter": 128,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa maoni yangu juu ya ripoti zilizowasilishwa na kamati mbili muhimu; Kamati ya Ardhi na Kamati ya Leba . Kuhusiana na Kamati ya Leba, ni ukweli, maendeleo ambayo yamefanyika ni mazuri kwa Kamati na Bunge letu la Seneti. Lakini ni masikitiko kwamba imechukua muda kidogo kuweza kukamilisha ile ripoti inayohusiana na shida wanazopitia wafanyikazi wetu ambao wako katika nchi za Uarabuni, hususan Saudi Arabia na nchi zingine za Ghuba. Safari ilifanywa mwezi wa Januari tarehe 7 na kufikia sasa ni karibu miezi mitatu imepita na hatujaweza kukamilisha ripoti hiyo. Kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yamezungumziwa katika safari ambayo tulifanya kule Saudi Arabia na vile vile kamati ambayo ilikuwa inahudumu katika maswala ya leba mwaka 2017/2022 walikuwa pia wamefanya ziara katika nchi hiyo lakini masikitiko ni kwamba yale ambayo walipendekeza kutekelezwa hayajatekelezwa na Wizara pamoja na taasisi zingine za Serikali. Ningeomba kwamba Kamati iharakishe swala hili kwa sababu ni swala ambalo liko hai kila siku. Kila siku tunapata ripoti kama hizo na itakuwa si vizuri wakati sisi tunakaa hapa na tunaacha mambo kama hayo yanaweza kupita. Asante."
}