GET /api/v0.1/hansard/entries/1229043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1229043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229043/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Madazyo, lakini hakuna jambo lolote limetendeka. Ni kama kazi yetu hapa ni kuongea tu lakini hakuna mapendekezo yoyote ambayo yanafuatiliwa. Si hilo peke yake. Kuna wafanyikazi ambao wanasononeka kila wakati. Hao ni wale ambao wanaenda katika nchi za Uarabuni. Mambo ambayo tumekuwa tukiongea hapa ni yale yale. Tunapoongea, ni kama mapendekezo tunayotoa yanachukuliwa na Mwenyekiti ambaye hungoja muda wake uishe kisha amkabidhi mwingine anayekuja baada yake bila mapendekezo yoyote kutekelezwa. Wenyeviti huwa wanafanya juhudi na kuzuru sehemu ambazo wanapaswa kutembelea. Hata hivyo, ni kama mapendekezo ya Kamati huwa yanawekwa katika kabati na kuozea au kupata vumbi huko na hakuna lolote linatekelezwa. Kwa hivyo, kile ambacho tungependa ni Waziri--- Nashukuru Serikali ya Kenya Kwanza chini ya uongozi wake Mhe. William Samoei Arap Ruto kwa sababu Mawaziri watakuwa wakija katika Bunge hili kujibu maswali. Waziri anayehusika atakuwa anajibu maswali. Tutakuwa na nafasi ya kumwuliza peupe ili atuelezea pale alipofikisha mambo ya madiwani. Madiwani wanasononeka na kupata shida. Wengine wameandikwa kuchunga. Ukitembea katika Kaunti ya Laikipia, utapata kuwa waliokuwa madiwani wameandikwa kuchunga. Ukienda katika Kaunti ya Kitui, utapata kuwa hao ndio wachimba migodi. Waziri atakayekuja hapa anafaa kujibu hayo maswali magumu. Nashukuru na kumpongeza Rais kwa kukubali Mawaziri wawe wakija hapa ili tuwaulize maswali, badala yao kujibu maswali kupitia kwa Wenyeviti wa Kamati."
}