GET /api/v0.1/hansard/entries/1229142/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229142,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229142/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada ambao umeletwa Bungeni na Sen. Mungatana, MGH, Seneta wa Kaunti ya Tana River, kule ambako mamba wanashindana na wananchi kwa huduma za maji. Mswada huu ni muhimu sana ikizingatiwa kwamba Katiba yetu ya mwaka 2010 iliweka bayana haki za jamii - social rights na haki za kiuchumi - economic rights . Kifungu cha 43 cha Katika ya Kenya kinatoa wazi haki hizo, zikiwemo haki ya afya bora pamoja na haki za kimsingi za kuzaa, haki ya kuwa na nyumba ama makaazi ya kuishi, haki ya kuwa na hali ya juu ya usafi, haki ya kupata chakula cha kutosha na chenye virutubisho vyote, haki ya kimsingi ya lishe kwa watoto, haki ya kuwa na maji safi ya matumizi na kwa wingi, na haki za kijamii kama vile ruzuku zinazotolewa kwa jamii tofautitofauti ambazo hazijiwezi. Pia, tuna haki za elimu. Haki hizi zote ni muhimu na ni za kimsingi. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba, hata zile haki za kibinadamu za kimsingi, tumeona kwamba bado zinahujumiwa na Serikali yetu ya sasa. Kwa mfano, hivi majuzi, haki ya kuandamana; haki ya kupeleka stakabadhi kwa ofisi za kiserikali ilihujumiwa pakubwa wakati hata Wabunge na Maseneta walishikwa kwa kutekeleza haki hiyo. Haki hizi zote zitakuwa ni ndoto mpaka pale Serikali itakapoona kwamba kuna umuhimu kwanza wa kulinda haki ya binafsi ya kimsingi ya maisha. Tumeona watu kadhaa waliuliwa katika maandamano ambayo yalikuwa ya amani. Tumeona kwamba itakuchukua muda mrefu sana kuweza kuzipata haki hizi iwapo Serikali itakuwa bado na zile fikra potovu kwamba maandamano yoyote ni maswala ya fujo. Kwa hivyo, watu wapigwe na kufukuzwa ili wasitekeleze azima yao ya kuandamana. Tukiangalia, ijapokuwa ugatuzi umeweza kusongesha mbele haki hizi, tumeona, kwa mfano, kaunti tofauti zimeweza kujenga zahanati na hospitali za kisasa, wameweza kurahisisha kupatikana kwa maji safi. Kuna kaunti nyingi ambazo zinatoa ruzuku kwa watoto ama lishe kwa watoto wanaokwenda katika maeneo yale ili waweze kupata chakula. Hata wale ambao wanasoma shule za msingi au chekechea wanapata lishe ili wasisafiri kuenda makwao kupata chakula cha mchana wakati wameenda shule. Ijapokuwa kaunti nyingi zimeweza kufanya hivyo, hali hii pia inahujumiwa kwa kucheweleshwa kwa zile ruzuku ambazo zinapelekwa katika kaunti hizi kila mweli kulingana na sheria. Kwa mfano, katika Kaunti ya Mombasa, pesa za mwisho zimepelekwa na Serikali kuu mwezi wa Disemba Mwaka jana. Hiyo inamaanisha kwamba zile huduma zote ambazo kaunti ile ilikuwa imepanga kufanya, kwa mfano, kupeleka lishe kwa watoto, kuleta maji safi kwa wananchi, zote zimmelemaa kwa sababu ya upungufu wa fedha."
}