GET /api/v0.1/hansard/entries/1229144/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229144,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229144/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, tukiangalia wakulima, hivi majuzi Serikali ilileta mfumo wa kuleta mbolea. Ijapokuwa ni jambo nzuri, ni jambo la kushangaza kwamba Serikali yetu imetoka hapa mpaka nchi ya Zambia kuenda kuwasaidia wakulima nchini humo kuzalisha mahindi mengi ili walete Kenya wakati hatujaweza kuwahudumia wakulima wetu kikamilifu. Badala ya kuwa na vipimo vya kupima Zambia, tutaleta mahindi ama tutaleta mazao kiasi gani, tuwe na vipimo vyetu hapa Kenya ili kuona kwamba wakulima wetu wote wanazalisha chakula cha kutosha ili kulisha nchi yetu ya Kenya. Katika maswala ya maji, kunajengwa mabwawa kila mara lakini tatizo sugu la maji bado halijatatuliwa. Kwa mfano, tukiangalia sehemu za pwani hususan Mombasa, maji tunayoyapata ni yale ya Mzima Springs ambayo ilijengwa katika mwaka 1945. Katika miaka kumi na tano au ishirirni inayokuja, itakuwa Mzima Pipeline inasherehekea karne moja na hatujaweza hata kuunganisha pipe moja kutoka Mzima kuelekea Mombasa ama Taita ili tuweze kupata Mzima 2 ma Mzima 3. Bw. Naibu Spika, sheria hii ambayo imebuniwa inakuwa na umuhimu kutekeleza lakini la kusikitisha ni kwamba, hata zile taasisi ambazo ziko kwa sasa, kwa mfano Kenya National Human Rights Commission (KNHRC) ambayo inatakikana kuchunguza matukio ambayo yanahujumu haki za binaadmu yameshindwa kufanya hivyo kikamilifu. Hivi majuzi, tuliona watu wakipigwa wakiandamana, na maandamano yametibuliwa bila kufuata sheria lakini hata siku moja hatukusikia KNHRC ikizungumzia swala hilo ambalo Katiba inalikubali. Mwongozo uliotolewa katika sheria hii utasaidia pakubwa lakini hautoshi kwa sababu zile taasisi nyingi ambazo tunaziuunda zimelemazwa kutokana na State capture . Tukiangalia, tume huru nyingi ziko na watu ambao ni vikaragosi ama vibaraka wa Serikali iliyoko mamlakani. Hivyo basi, wanashindwa kutoa ripoti muhimu ama kuzungumzia mambo muhimu ambayo yanatokea kwa sababu ya kuogopa na kusikitikia nafasi zao."
}