GET /api/v0.1/hansard/entries/1229291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229291,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229291/?format=api",
    "text_counter": 35,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kassim Tandaza (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Matuga, ANC): Asante Mhe. Spika. Kwanza, ni huzuni kumpoteza mwenzetu ambaye tumekuwa naye kutoka kipindi cha Bunge lililopita. Pia ni funzo kwetu sisi ambao tumebaki kwamba kifo huwa hakitoi notice kama vile tunatoa wakati tunapohitaji mtu. Sote tuwe tayari wakati wowote tukijua tunawezaenda. La muhimu zaidi, tujue kwamba sisi sote tunaishi kwa huruma za Mwenyezi Mungu na hakuna haja kamwe kujigamba ukiwa hai kwamba unaweza na bila wewe haiwezekani kufanyika jambo fulani. Tujue kwamba tukiwa hapa, wakati tutakapoondoka maisha yataendelea. Ni wajibu wetu kuona kwamba wakati tuko hapa tuweze kutendea haki umma wote ndiyo tukienda mbele ya Mwenyezi Mungu naye pia aweze kutuhurumia."
}