GET /api/v0.1/hansard/entries/1229310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1229310,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229310/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gilgil, UDA",
"speaker_title": "Hon. Martha Wangari",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Bwana Spika. Hata mimi ninaungana na wewe na wenzangu kutoa rambirambi zangu binafsi na kwa niaba ya watu wa Gilgil kwa watu wa Banissa na jamaa na marafiki wa mwendazake, Mheshimiwa Kulow. Wale ambao walifanya kazi naye, haswa katika Bunge lililopita, wanajua kuwa alikuwa mtu ambaye hakuwa na maneno, na mwenye tajiriba na ujuzi mwingi. Alikuwa mwalimu na mnyenyekevu na tulifanya kazi bila vita au vurugu yoyote. Wale ambao walikuwa naye katika kamati mbalimbali wanajua kuwa hakuwa na maneno mengi. Alikuwa mpole na alipendwa sana na watu wake. Ukiangalia vile alivyoingia Bungeni, sio kutokana na vyama vikubwa. Alikuwa na ujuzi wa watu wa Banissa. Ninaungana na wenzangu kuomba Mungu airehemu roho yake na amuweke mahali pema. Kwa watu wa Banissa, tunawapa pole. Kwa jamaa na marafiki, Mungu awafariji."
}