GET /api/v0.1/hansard/entries/1229323/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229323,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229323/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Bw. Spika. Kwa niaba yangu na ya watu wa Taita Taveta na Pwani yote kwa jumla, ninaungana na wenzangu kutoa rambirambi kwa familia ya Mheshimiwa Kulow, watu wa Banissa na Mandera yote nzima. Kwa kweli tumepoteza kiongozi aliyekuwa mkakamavu na mpenda watu. Mahusiano yake na watu yalikuwa mazuri sana. Hii inatufunza kwamba tunapoishi katika hii dunia, tujue maisha ni ya Mungu na basi tutengeneze mahusiano yetu hapa duniani. Vilevile, ninachukua hii fursa kutoa rambirambi zangu kwa watu wa Kishushe kule Taita Taveta, ambao wamepumzisha watu wanne leo waliofariki kupitia mafuriko yaliyotokana na mvua iliyonyesha hivi juzi. Pole zangu kwa watu wa Kishushe na watu wa Mwatate kwa jumla. Ahsante sana Bw. Spika."
}