GET /api/v0.1/hansard/entries/1229625/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229625,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229625/?format=api",
    "text_counter": 369,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": "Ningependa kumpongeza Kiongozi wa Walio Wachache, Mhe. Opiyo Wandayi, kwa kuileta Hoja hii. Ni dhahiri shahiri kuwa Wakenya wanahangaika. Hivi leo mnasema kuwa yale maandamano yalifanya uchumi ukawa mbaya, lakini kwa kweli huo ulikuwa ni ujumbe kwenu kuwa Wakenya wamechoka. Huo ndio ujumbe. Hawa ndio walipaushuru lakini hadi leo wanakosa mishahara. Wabunge tumekaa mwezi bila kulipwa mshahara. Ni dhahiri shahiri kuwa wale wengi wanaongea kutoka kwa mifuko yao. Hali ya uchumi imekuwa mbaya na kuna wakati ambapo mijadala ya dharura huletwa humu Bungeni ili ijadiliwe. Kusema kuwa tupeleke mambo huku na huko itakuwa si sawa. Wakenya wanahangaika. Ningependa kuwaeleza kuwa kushiriki maandamano na kuzungumza katika Bunge hili ni mambo yanayokubalika katika Katiba. Ningependa kuwaambia wale ambao wanasema kuwa wafuasi wa Azimio la Umoja walienda maandamano na watu wakafa kuwa watu hao waliuawa na polisi ambao wako kwenye Serikali. Nchi nyingi kama vile South Afrika…"
}