GET /api/v0.1/hansard/entries/1229644/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229644,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229644/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaunti ya Mombasa, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Mshahara ulichelewa. Wafanyakazi wa kaunti pia ni wafanyakazi wa serikali na mpaka sasa wengi wao hawajalipwa. Tusiseme sisi Wabunge peke yetu ndio wafanyikazi wa serikali. Kenya iko katika hali tata sana. Ningependa kuwaelezea wenzangu kuzingatia na kuchuja maneno tunayozungumza kule nje ama tutaweka Kenya kwenye moto mkubwa sana. Mambo ya kutulizwa yatulizwe. Sisi hatukuelezea viongozi wetu wakutane waongee; waliamua wenyewe. Tuwape heshima, wakae chini wazungumze. Tuwache kurusha maneno ovyo ovyo huko nje."
}