GET /api/v0.1/hansard/entries/1229904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229904,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229904/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwa mara ya kwanza, nitajaribu kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili. Natumai kwamba sitafeli. Ningeanza kwa kumpa kongole Mbunge wa Githunguri, Mhe. Gathoni Wamuchomba, kwa sababu ya kuwafikiria wanafunzi wetu katika shule zetu. Wakati tunasema ya kwamba masomo ni ya bure, ni wazi tunasema uongo. Wakati tunasema ya kwamba masomo ya zile shule za kila siku ni bure, ama kwamba hakuna karo inalipwa huko, tunajua huo ni uongo. Tunaposema ya kwamba inawezekana kupeleka watoto katika shule za mabweni kwa wale wazazi wa hali ya chini, jibu ni kwamba huo pia ni uongo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}