GET /api/v0.1/hansard/entries/1229905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1229905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229905/?format=api",
    "text_counter": 138,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": "Wakati nilikuwa kule mashinani Molo siku ya Jumapili, nilipatana na mama mmoja ambaye anauza sokoni. Mtoto wake alikuwa ameitwa Shule ya Upili ya Karoti kule Kirinyaga. Yule mama alikuwa na risiti ya kuonyesha ya kwamba ameweza kulipa karo ya Ksh20,000 lakini, juu ya hiyo, alihitajika kulipa pesa zingine Ksh20,150 ya zile bidhaa ambazo zinahitajika pale shuleni ambazo alishurutishwa asinunue mahali pengine ila kule shuleni. Huyu mama ametia bidii. Kwa yule mama ambaye anauza nyanya sokoni kuweza kuweka Ksh20,000 ili aweze kumpeleka mtoto shuleni, ni juhudi kubwa sana. Aliponiambia kwamba amelipa karo, nikamuuliza kama alitafuta bursary . Aliniambia kwamba bursary haitaweza kulipa hayo mahitaji mengine. Ilibidi nitafute hela zangu kibinafsi ili niweze kumlipia, ili mtoto wake aweze kusoma. Ninafurahia ya kwamba huyo msichana ameanza maisha yake ya kidato cha kwanza katika shule ya Karoti kule Kirinyaga. Jambo hili lilinifanya nianze kufikiria: Hizi Ksh20,000 ambazo alikuwa anaitishwa ni za nini? Ukienda sokoni, shati ya shule ni Ksh350. Ukienda kuinunua hiyo shati kule shule ni Ksh800. Wanaongeza Ksh450, mara tatu ya zile pesa ambazo hiyo shati inagharimu huku nje. Vile vile, ile suruali ukinunua huku nje ni Ksh700, ilhali shule nyingi wanaziuza kwa Ksh1,500. Ukinunua fulana dukani ni Ksh750, lakini shule inauza Ksh1,500, mara mbili ya bei ambayo ungenunua huko nje. Tai ya kawaida ukinunua sokoni ni Ksh150, ila ukienda kununua kule shule ni Ksh300. Tena wanasema ununue ile track suit . Ukiinunua dukani ni Ksh1,300, na ukienda kuinunua kule shule, wanauza kati ya Ksh2,000 na Ksh3,000. Godoro la kulalia, ukilinunua kwa duka ni Ksh1,800, ilhali mashule yetu yanaitisha wazazi pesa za kununua lile godoro, ambalo linakuwa hata ni dogo Ksh2,800. Ingine ambayo wanaiita fulana ya kuruka, ya mtumba unaweza kupata na Ksh200, lakini kule shuleni wanaitisha Ksh2,500. Blanketi ukiinunua kwa soko ni Ksh500, lakini ukienda kuinunua shuleni, wanaitisha katikati ya Ksh700 na Ksh1,000. Vile vile, ile shuka ya kutandika kitandani, kwenye maduka ni Ksh600, ilhali shuleni ni Ksh1,000. Mto wa kulalia ukiununua kwa soko ni Ksh150, lakini shuleni wanaitisha kati ya Ksh300 na Ksh500. Na hakuna tofauti ya ule mto ambao uko kwenye soko na unaoitishwa na walimu wetu katika mashule. Ndoo ya kubebea maji au ya kusafisha nguo kwa soko ni Ksh150, ilhali shuleni ni kati ya Ksh300 na Ksh500. Zile soksi ukinunua dukani ni katikati ya Ksh50 na Ksh100. Waalimu wanaitisha katikati ya Ksh200 na Ksh500. Juu ya hayo, wanakuambia baada ya kulipa hizo pesa zote, kuwa lazima ulipe katikati ya Ksh500 na Ksh1,000 ili kuweka alama katika zile sare za shule. Kwa hivyo, ikiwa tunataka mtoto wa Mkenya yeyote aweze kwenda shuleni aweze kusoma na kufaulu katika maisha, itabidi kuhakikisha ya kwamba tumeongeza pesa za ufadhili katika shule zetu. Lazima tupeane suluhu ya sare za shule na haya mambo mengine yote ambayo yanahitajika katika shule zetu. Njia rahisi kabisa ya kufanya hivyo ni kuhakikisha ya kwamba sare zote za shule za umma katika nchi yetu ya Kenya ziwe sawa. Shati iwe ni ya rangi nyeupe. Kama ni suruali, iwe rangi nyeusi au kijivu. Kuwe na kiwango kimoja kote nchini. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumesaidia kupunguza gharama ya shule na, zaidi ya hayo, tutakuwa tumehakikisha ya kwamba yule fundi ambaye ako pale Mukinyai, Kapsinendet, Chandera, Arimi na Kapsita, anaweza kushona hizo sare za shule na kusomesha watoto wake na kuweka chakula kwa meza. Tumekuwa tukitengeneza sheria ambazo ni za kuhahikikisha ya kwamba wale mabwenyeye tu ndio wanaweza kunufaika kutokana na hizo sheria. Kwa mfano, hata ukiangalia shule zetu ambazo ziko mahali kwingine, unapoambiwa hii ndio barua ya kukaribishwa shuleni, unaambiwa zile sare za shule lazima ununue kwa maduka fulani. Siyo ya kwamba hayo maduka mengine hayana hizo sare; sio ya kwamba bei yao ni nzuri kuliko maduka mengine; lakini unashurutishwa hivyo kwa sababu kuna lile agano ambalo mwalimu amefanya na hilo duka maalum. Na unapata hayo maduka hayana mali tofauti na mengine. Ni vile tu hao ni mabwanyenye, na wameweza kujikimu kimaisha. Ndio unapata wale ambao The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}