GET /api/v0.1/hansard/entries/1229906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1229906,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1229906/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": "wako na hela katika nchi hii wanaendelea kupata zaidi na wale ambao hawana, wanaendelea kukosa zaidi. Kuna wale ambao waliongea hapa awali wakasema basi kama sare zote za shule zitakuwa za rangi moja, pengine hakutakuwa na umaridadi. Nakumbuka ya kwamba yule ambaye alikuwa Daktari Matiang’i alikuwa na makosa mengi sana. Alifanya mambo mengi mabaya lakini kama kuna jambo moja alifanya nzuri, ni kusema ya kwamba basi zote za shule katika Kenya ziwe za rangi moja. Unamkumbuka yule ambaye alikuwa Waziri wetu wa Uchukuzi – na apumzike kwa amani Marehemu Mheshimiwa Michuki - alisema kwamba wale ambao ni madereva na makanga wa magari yetu wavae sare moja - wengine zile za rangi ya maroon na wale wengine wavae rangi ya blue kwa madereva. Ukienda kwenye eneo lolote la uchukuzi katika nchi yetu, utaweza kujua huyu ni dereva na huyu ni makanga. Na pia, kwa kununua zile sare, unaweza kuzinunua mahali popote katika nchi yetu. Ni nini ambalo tunalipendekeza hapa? Katika shule zetu za kufunza elimu ya matibabu ambayo tunaiita Kenya Medical Training College (KMTC) kwa lugha ya kimombo, hilo limewezekana. Hiyo ni kwa sababu yule msichana au mvulana ambaye anasomea KMTC ya Molo, Kitui, Kisumu, Mombasa, Lamu na kila mahali, wako na sare moja. Kama basi inawezekana hivyo kwa mashule yetu ya matibabu, mbona basi isiwezekane kwa mashule yetu ya upili na ya msingi katika Jamhuri yetu ya Kenya? Inawezekana! Lakini hapa tukubali ya kwamba halitakuwa jambo rahisi kwa sababu, tukienda kupitisha hili, litakataliwa kwa njia kubwa sana. Tukiongea kule, lazima pia nizungumzie mambo ya vitabu ambavyo vinapelekwa katika shule zetu. Tunasema ya kwamba tunanunua vitabu vyote katika shule haswa za upili, lakini wanaitisha Bibilia, kamusi na vitabu vingine. Hivyo vitabu peke yake ni Ksh5,000. Kama tunaweza kununua hivi vitabu vingine hadi shule zingine ziko na vitabu zaidi, mbona basi tusinunue na kuwapa wanafunzi wetu, ili huyu mtoto wa masikini katika nchi yetu ya Kenya awe na nafasi sawa ya kusoma na kufaulu katika maisha kama wa tajiri? Nakushukuru, Mhe. Spika wa Muda."
}