GET /api/v0.1/hansard/entries/1230297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230297,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230297/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kuria East, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda kwa nafasi hii nzuri ya kipekee ya kuafiki Hoja hii ambayo imeelezewa katika Nyumba hii kwa namna ya ufasaha kabisa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maji. Kamati hiyo vile vile inaangalia mambo ya unyunyizaji wa maji na ukulima wa ndani ya bahari, zikiwemo fuo za bahari. Kamati hii inaangazia mambo yanayohusiana na uchumi samawati. Mheshimiwa Martin Otieno Ogindo alikuja mbele ya Kamati yetu na tukazingatia sheria za nchi ambazo zimetungwa na Bunge na yale yote ambayo ni muhimu. Alionekana kuwa anafaa achukue nafasi hiyo ambayo ameteuliwa na Mheshimiwa Rais ili aisukume nchi hii, haswa upande huu wa uchumi samawati. Alikuja mbele yetu na tukamhoji. Alipendeza katika mazungumzo yake. Ni mtu ambaye amesoma. Masomo yake si ya juu juu. Ni masomo ambayo yamefikia kilele chake kabisa. Kama Kamati, tulijitosheleza na maelezo aliyotoa Mheshimiwa Martin Ogindo na ufahamu wake wa mambo yanayohusiana na uchumi samawati, uvuvi, na sheria zote ambazo zimependekezwa kusaidia sekta hii iweze kutoa ajira na kuhakikisha kuwa nchi hii imepata rasilimali na uchumi samawati ambao umekomaa. Kwa hivyo, tulisadiki maelezo yake. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Martin Otieno Ogindo, ambaye ni mwenyeji na mkaazi wa Homa Bay, kwa sababu ni shemeji yangu. Ni vizuri niseme kuwa nimeoa katika Kaunti ya Homa Bay na ameweza kusimamia watu wa maeneo hayo na kuonyesha kwamba anaweza kufanya hiyo kazi. Watu wa eneo hilo kwa wingi shughuli zao ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}