GET /api/v0.1/hansard/entries/1230311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230311,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230311/?format=api",
    "text_counter": 330,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Amina Mnyanzi",
    "speaker": null,
    "content": "Ninamkaribisha kwa mikono miwili na kumpatia baraka zetu. Ninaomba viongozi wenzangu kumuunga mkono. Uchumi samawati ndio unazungumziwa dunia yote hivi sasa. Kule Pwani tuko na samaki wengi. Soko yao haijapatikana hapa Kenya, bara la Afrika na dunia nzima. Ndiyo maana nataka tufanye kazi pamoja na ndugu huyu. Kule Pwani kuna samaki wanaitwa red snapper, ambaye anauzwa Ksh500 kwa kilo moja. Kilo ya samaki ya prawns ni Ksh1,200. Mhe. Spika wa muda, kuna pweza, tuna, na lobsters ambao wako na bei nzuri na tunaweza sisi tukafanya mauzo mema ili kuinua uchumi wa Kenya yetu. Ni wakati sisi kama Wakenya tuanze kuzungumza kuhusu maswala ya samaki. Samaki wanatusaidia sisi, afya yetu na kwa wale ambo hawajui, kuna huyu samaki ambaye anaitwa pweza. Nafikiri wengi wenu mnamjua. Kwa wale ambao hawajui umuhimu wa pweza, mnifuate baada ya Bunge niwaambie maana ya pweza ni nini. Ndio maana ninasema tuzingatie umuhimu wa samaki katika Kenya. Asante Mhe. Spika wa muda."
}