GET /api/v0.1/hansard/entries/1230319/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230319,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230319/?format=api",
"text_counter": 338,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Usambazaji na Uuzaji wa Samaki. Nilikuwa kwa kamati ambayo iliweza kuzungumza naye na tukaona ni mtu ambaye anatajiriba inayofaa. Ukiangalia masomo yake, sio ya kubahatisha. Mhe. Martin Ogindo ni mtu ambaye alisomea shule ambazo zinatajika hapa Kenya mojawapo ikiwa ni Alliance High School. Kwa hivyo, moja kwa moja tunaona kwamba ni mtu ambaye huwezi kubahatisha makaratasi yake na kuyapiga msasa mara mbili tatu. Lakini moja kwa moja tulijua ni mtu ambaye anazungumza, anafanya, anatenda na anauadilifu kulingana hata na ule msingi ambao alikuwa nao akiwa shule ya upili. Pia, ukiangalia ile taaluma yake ya uhasibu, inafaa sana katika ofisi hii ambayo ameweza kuteuliwa. Kulingana na maswala tulioweza kumtahini, tuliona ni mtu ambaye ataweza kuleta ufahamu na mbinu mpya mbadala ambazo zitaweza kukuza sekta hii ya samaki. Ningependa nizungumuzie kwa kina kidogo juu ya samaki. Ni jambo ambalo limeweza kuregesha nchi nyuma kutoka tupate uhuru. Tukizungumzia samaki mara nyingi, tunaangalia upande ule wa Ziwa Victoria. Tukijua kwamba tumemiliki asilimia sita peke yake ya lile ziwa. Kwa hali yoyote hatuwezi kuwa na samaki wa kutosha kutumia hapa nchini na hatimaye kuweza kupeleka nchi za ughaibuni. Pia, baada ya hapo, tukakuwa na Wizara ya Samaki, lakini la kuhuzunisha ni hatukuweza kuboresha samaki ambao hawana gharama yoyote walio katika Bahari ya Hindi, ambapo tuko na karibu kilomita mia sita na kuenda ndani kama sikosei zaidi ya kilomita zingine mia mbili. Samaki hawa ni bure, hawalishwi, hawana gharama na hawapatiwi dawa wala chakula. Lakini la kuhuzunisha ni kwamba Wizara ya Samaki ilipobuniwa ikawa inaenda kuchimba vidimbwi ambavyo vina gharama. Kuwambia watu wanunue chakula cha samaki ndio walishwe na kuuzwa. Jambo hili linatendeka ilhali kuna samaki ambao unahitaji ndoana, mtumbwi ama boti la kisasa uweze kuwapata bure, kutumia na kuuza. Samaki hawa kwa sababu serikali iliopita haikuweza kuitilia nguvu, imeishia kwamba ndio wanaovuliwa na Wachina kama tulivyosikia hapa na baadaye tunauziwa sisi ikiwa ni raslimali yetu. Kwa hivyo ni tamaa, maoni na matumaini yangu kwa Bwana Martin Ogindo ambaye anapatiwa nafasi hii sasa, kuweza kuangazia hasa, maeneo ya Pwani ambapo tuna samaki ambao hawana gharama yoyote. Sioni ikiwa tutakuwa tunatumia fedha za mwananchi vizuri kugharamia kukuza samaki ilhali tuna samaki tayari ambao mwenyezi Mungu ametubariki katika nchi hii yetu. Tusisahau samaki hawa ambao wako maeneo ya baharini, pia mbali na kuwa chakula, kuna wale ambao ni dawa. Wanaweza kutusaidia sana katika nchi hii hasa wazee ambao wako katika Bunge hili na wengineo. Ukiangalia samaki kama vile pweza na ngisi najua kwamba watu wengi wanapoweza kuja maeneo ya Pwani hutafuta supu ya samaki hawa kwa sababu ni dawa ya bure. Badala ya kununua madawa ghali ambao mara nyingi unaskia labda kuna mtu ameweza kuzimia na kupoteza maisha yake akiangaliwa.... Askari wakikuja wanapata kulikuwa na vidonge sijui vya rangi ya buluu. Kihistoria hakujawahi zungumziwa kwamba yule amepata tiba ya supu ya ngisi ama supu ya pweza ameweza kuzimia na kupoteza maisha yake. Bwana Martin Ogindo tulipokuwa tunamutahini, tulimuuliza kama anajua tiba kama hizi za kiasili za bure ambazo hazina madhara yoyote na akakubali kwamba anazifahamu. Basi katika kukuza, sio tu kwa sababu ya kupeleka nje lakini kwanza nikufanya utafiti zaidi ya kuona ni vipi samaki hawa wanaweza kuwekwa katika mitambo. Waweza kuhifadhiwa na kusambazwa kila mahali na wale walio na matatizo na madaktari wetu waweza kuwafanyia utafiti na kuona labda mbali na kunywa supu, watatengeneza tembe lakini ziwe hazina madhara yoyote. Kwa hivyo, katika swala zima la samaki tuko na uchumi ambao unaweza kusaidia nchi hii, ikiwa serikali ambayo ina imani kwa kuteua Mhe. Martin Ogindo imeweza kugundua hivyo, basi watilie mkazo maeneo ya Pwani. Moja kwa moja hii itaweza kuleta ajira, fedha za kigeni na hasa upande wa utafiti wa tiba itaweza kusaidia. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}