GET /api/v0.1/hansard/entries/1230337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230337,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230337/?format=api",
    "text_counter": 356,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii adimu kumzungumzia Mwenyekiti wetu mpya ambaye ameteuliwa kusimamia Kenya Fish Marketing Authority. Ninachukua fursa hii kumpongeza sana Mhe. Martin Ogindo. Nikiangalia maelezo yake, alikuwa mwenzetu katika hili Bunge na kiongozi mchapa kazi. Nikiangalia masomo yake pia, anastahili kupata cheo hiki kwa sababu amefanyia taifa hili mengi. Ninampongeza sana na ninamkaribisha kwenye soko la samaki. Kama mama Mombasa, sote tunajua kuwa sehemu kubwa ya blue economy imeshika sehemu ya Pwani. Wavuvi wetu ni kati ya watu maskini sana katika taifa hili. Wanaingia baharini wakati wa baridi kuvua samaki lakini wakishawatoa nje, hawana soko. Unapata mvuvi ametoa samaki wa kutosha lakini atakaa nao bandarini maana hakuna mnunuzi na samaki wanaharibika. Ninataka nimueleze ndugu yetu Mhe. Martin ambaye ni mwenyekiti wetu kwamba aangalie wavuvi wetu na ahakikishe wanapata vifaa vya kuvulia samaki. Alivyosema mmoja wetu hapa, ni kweli kuwa wanahitaji majahazi ya kuingia baharini kuvua samaki. Wakiingia na mitumbwi kule baharini, maskini wengine hawatoki kwa sababu ya yale maji yalivyo mazito. Yanapiga ilhali wana mitumbwi tu kwa sababu ndicho kitu wameweza kupata katika hali yao duni ya maisha. Ninamweleza ndugu yetu Mhe. Martin ambaye ni mwenyekiti mpya aangalie wavuvi wapate madau ya kuwawezesha kuingia ndani kabisa kuvua samaki."
}