GET /api/v0.1/hansard/entries/1230338/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230338,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230338/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ambalo ninataka kumweleza ni kuwa nilipoangalia stakabadhi au Ripoti hii, imenihakikishia kuwa mwalimu wangu aliyenifunza jiografia katika Kenya Methodist University (KEMU) alinieleza mambo ya kweli. Nimeyathibitisha kufwatana na Ripoti hii ya leo. Ripoti hii imeonyesha hakika kuwa Uchina wanavua samaki zetu kwa wingi sana katika maji makuu. Ni sehemu iliyo katika anga za Kenya. Ni sehemu iliyo katika taifa la Kenya. Ninamweleza ndugu yetu Martin ambaye ni mwenyekiti afuatilie serikali kuhakikisha kuwa sehemu yetu ya Wakenya kuvua samaki iwe yetu wenyewe na tuuze samaki wetu humu nchini Kenya na kule nje. Mchina anavua katika anga zetu. Anavua samaki kwa wingi sana kisha anakuja kutuuzia. Najiuliza swali: Kama si ujinga ni kitu gani? Mtu aje shambani mwako, avune mazao yako, kisha akuuzie kwa bei ghali nawe umenyamaza. Ni wakati wa Serikali kuchukua hatua. Tuangalie kuwa kama vile Wachina wanatoa ulinzi katika anga zao, anga zetu za Kenya zilindwe. Wavuvi wetu wamekuwa maskini miaka mingi. Ni wakati watambulike katika taifa hili, wapewe sehemu yao inavyohitajika ili tuone uchumi wa Kenya ukipanda juu."
}