GET /api/v0.1/hansard/entries/1230344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230344,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230344/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo lingine ninalotaka kuzungumzia ni kuwa sehemu ya kuhifadhi samaki imekuwa donda sugu kwa wavuvi wetu. Wanavua samaki wengi lakini mahali baridi pa kuweka samaki pamekuwa adimu kwao. Utapata wengi wamekaa kando ya bahari na samaki wao wakisema “nisipouza leo, kesho samaki watakuwa wameharibika na watoto wangu hawatapata chakula”. Ninamuomba mwenyekiti mpya wa uvuvi ahahakikishe kuwa Beach Management Unit wamepewa sehemu za kuhifadhi samaki kando ya bahari na sehemu nyingine za soko."
}