GET /api/v0.1/hansard/entries/1230345/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230345,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230345/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Ninaeleza Serikali kuwa soko la samaki ni muhimu sana katika taifa hili. Wavuvi wengi sana kule Kisauni walinifuata kama mama kaunti wakaniambia “mama, tunaomba tujengewe soko la samaki”. Wanaomba kwa sababu wengi hawajulikani kama wanasamaki. Wamevua lakini pengine jirani zao pekee ndio wanajua. Laiti wakipata soko la kuweka samaki, itaaminika kuwa lile soko pale ndilo soko la samaki na kila mmoja atawania kwenda kununua. Mhe. Spika Wa Muda, jambo lingine ni kuwa tuangalie sehemu na viwanda vya samaki. Kutoka tuelezewe vinajengwa, hatuoni vikimalizwa. Serikali imekuwa na uvivu sana katika biashara ya samaki. Ukiangalia hata ile inajengwa pale Liwatoni, bado halijamalizika. Kuna nyingine Malindi. Kuna moja kule Ngomeni, kule Magarini, na nyingi nyinginezo. Ningeomba wapatie masoko ya samaki kipaumbele wajenge viwanda tutapeleka samaki wetu. Tupakie samaki wa mikebe kama tuna na wengine. Ukitembea katika supermarkets, utapata tuna kutoka India, Uchina, na hata kutoka mataifa jirani ilhali tuna tuna hapa Kenya. Tuna tuna wetu hapa. Tuna ngege, mbuta na samaki kila aina ambao ni samaki watamu sana. Ningependa kumwambia Martin aboreshe soko la samaki kwa sababu yeye mwenyewe ameingia kufanya mauzo. Pia, ahahakikishe kuwa anawapa samaki wetu soko litakaloleta mazao hapa Kenya na kuinua uchumi wa Kenya."
}