GET /api/v0.1/hansard/entries/1230346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230346,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230346/?format=api",
    "text_counter": 365,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo lingine ni kuwa nilitaka kuzungumzia mambo ya usafi katika bahari zetu. Meli nyingi zitapita zikimwaga mafuta ya meli. Pia, kuna wale hutupa taka baharini. Hii inaweza kuregesha soko la samaki nyuma kwa sababu samaki wengi wanakufa baharini. Ndio maana Mheshimiwa mmoja amesema siku hizi utapata samaki wengi wamekufa lakini wako kando ya bahari. Imetendeka Mombasa pia na sehemu nyingine. Ni jambo linalotupa wasiwasi sisi kama Wabunge kwa sababu huwezi kutumia samaki waliokufa kwa sababu hatujui wamekufa kwa kula sumu ama kwa nini. Hivyo tunaomba waboreshe fuo zetu kwa kuhakikisha ni safi. Wajengee wavuvi vyoo na mahali pasafi. Wawape mavazi safi na mazuri ya kuwakinga na baridi kule baharini. Waangalie meli kubwa itakayoingia maji makuu kutoa samaki ili tupate samaki wetu kwa wingi. Ninaona muda hu nami. Hata hivyo, ninasema vifo baharini pia vimekuwa vingi. Tuangalie hawa wavuvi tuone kuwa wanapata mafunzo ya kujimudu wakiwa baharini ili wajue watatetea maisha yao vipi. Kwa hayo, asante, Mhe. Spika wa Muda. Napongeza sana mada hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}