GET /api/v0.1/hansard/entries/1230348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230348,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230348/?format=api",
    "text_counter": 367,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nami pia naungana na wezangu kumpongeza Mhe. Martin Ogindo kwa kuchaguliwa katika Kenya Fish Marketing Authority ambayo ni bodi ya kutafutia samaki wetu soko. Ninamfahamu kwa kuwa nilifanya kazi naye katika Bunge hili. Ninachukua fursa hii kusema tunatoka kule Mombasa ambako kuna wavuvi wengi sana. Shida kubwa ni biashara. Huwezi kufanya biashara bila mauzo kabambe. Mhe. Martin ambaye amechaguliwa kama mwenyekiti yuko na kazi kubwa sana kwa sababu wafanyibiashara wa samaki wana changamoto nyingi sana. Mfano mmoja ni kuwa hawana vifaa. Leo hii, huwezi kufanya marketing ama mauzo ya samaki ikiwa hujapata samaki. Huwezi kupata samaki kama hauna vifaa bora. Kwa hivyo, Mhe. Martin, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka hii, lazima awapatie nguvu wavuvi wa samaki ili awawezeshe kupata vifaa vizuri vya kuvulia samaki."
}