GET /api/v0.1/hansard/entries/1230354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230354/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Kulingana na wakati uliobaki, ningependa kuwaachia wenzangu nafasi wachangie Hoja hii. Twampongeza Mhe. Martin pamoja na timu yake. Wafanye kazi yao vizuri na wajue kuwa sisi, kama Wabunge, tunawaunga mkono kwa sababu tunamjua Mhe. Martin Ogindo. Tunajua tajriba yake ya kufanya kazi kwa sababu tumefanya kazi naye hapa. Hii ni awamu yangu ya tatu kama Mbunge wa Jomvu. Nimechaguliwa kutoka mwaka wa 2013 mpaka leo. Kwa hivyo, naijua hali ya Mhe. Martin. Tutafanya kazi pamoja na tushikane naye ili tuboreshe mambo ya uvuvi na samaki wetu."
}