GET /api/v0.1/hansard/entries/1230393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230393/?format=api",
"text_counter": 412,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Mvumilivu hatimaye hula mbivu. Nimevumilia, japo peke yangu upande huu, lakini wakati wangu umefika. Kwanza, nachukua nafasi hii kumpongeza Rais kwa kumteua Mhe. Martin Otieno kwa wadhifa huu wa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Soko la Samaki. Mhe. Spika wa Muda, ni matumaini yangu na Wakenya wengi hasa wavuvi kwamba watapewa hali nzuri ya ulinzi katika sehemu wanazomiliki. Nikizungumzia habari ya kisiwa cha Migingo, kuna wakati mmoja tulipitia sehemu hiyo. Lakini tulipata wavuvi wakihangaishwa na maafisa wa usalama wa Uganda. Ni matumaini yangu kwamba ndugu Martin Otieno, akiwa hapa, atahahakikisha kwamba wavuvi wetu wako salama kwa kupatiwa ulinzi na wale walinda usalama wa majini. Kuwe na maboti yatakayokuwa yakizunguka kuhakikisha wavuvi wetu wako salama. Si Migingo tu; kuna hata sehemu zile za Kismayu. Wavuvi wetu wengi wamepata kuteswa na maafisa wa usalama wa Somalia. Hivyo basi, ina maana kwamba maboti ya patrol ya kuzunguka maeneo yetu ya uvuvi yanahitajika kwa wingi. Ninavyozungumza, Malindi, Ngomeni, Marereni, na sehemu hizo zote hazina hata boti la kuwafuatilia. Sehemu hizi hazina mashua ya maafisa wa usalama kuhakikisha kwamba wavuvi wetu wako salama katika maeneo hayo. Vilevile, ni muhimu wavuvi wetu wapewe mashua na vifaa vya usalama. Mara nyingi tumepoteza wavuvi sehemu za Lamu kwa sababu wakati mwingine bahari huchafuka, na ikichafuka basi mawimbi huwa mazito."
}