GET /api/v0.1/hansard/entries/1230399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1230399,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230399/?format=api",
    "text_counter": 418,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ni ishara mbaya kwa mwenzangu kusimama nikiendelea, huku akileta hoja ya nidhamu pasipo kuwa na utovu wa nidhamu. Kuna haja ya kuhakikisha wavuvi wetu, wawe wa ziwani au baharini, wanapewa vifaa vya kutosha kufanyia kazi zao, hasa vifaa vya usalama ili iwapo bahari itakuwa ama ziwa itachafuka, basi waweze kujimudu. Hata ijapo mashua imezama, wawe wanaweza kuelea na kutoka nchi kavu. Vilevile, Kamati husika ikiongozwa na Mwenyekiti wao ilifanya vizuri maana ilitembelea sehemu yangu. Sehemu ile ipo kati ya bahari ambapo walikwenda kuchunguza ujenzi wa chumba cha kuweka mitambo ya kuhifadhi samaki. Wamefanya kazi nzuri. Vile vile, shughuli hiyo imepanua sehemu hiyo, kwa sababu stima imevutwa mpaka kule na wananchi wanaoishi kule watapata nafasi ya kupata stima majumbani mwao."
}