GET /api/v0.1/hansard/entries/1230400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230400/?format=api",
"text_counter": 419,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": "Hayo yote yakiendelea, kuna haja ya kusambaza huduma hizi kuanzia sehemu za Marereni na Kipini ili tuweze kujenga sehemu za kuhifadhi samaki. Samaki wengi wanapovuliwa huwa wanaozea huko baharini kwa sababu hakuna nafasi ya kuwahifadhi. Wakati mwingine, soko linakosekana na hivyo basi wavuvi wanaenda hasara. Nitaendelea kumpongeza aliyeteuliwa, Bwana Martin, na kumualika aende afanye kazi yake vizuri kama vile alivyowahudumia wananchi katika sehemu ile aliyokuwa amechaguliwa. Ni matumaini yetu kuwa atawahudumia Wakenya wote kwa jumla. Kwa hayo machache au mengi, ninaunga mkono uteuzi wake."
}