GET /api/v0.1/hansard/entries/1230485/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230485,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230485/?format=api",
"text_counter": 70,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ahsante, Bw. Spika. Ningependa nichukue nafasi hii kumshukuru Waziri kwa sababu amejaribu. Ninapozungumza hivi sasa, vita vinaendelea kwangu Baringo Kusini. Ninapozungumza hivi sasa, kijana mmoja amepoteza maisha yake na watatu wamejeruhiwa. Nimetuma pesa ya meli ya kuwapeleka hospitali wale ambao wameumia. Vile, nimetuma gari ya kuchukua mwili wa yule kijana aliyeuawa. Ng’ombe pia wameenda na watu wanakimbia na kuhangaika katika sehemu za Kiserian, Mukutani na Rugus. Ninajua Waziri alikuwa huko hapo awali, lakini ni uchungu kwamba kazi ya ujambazi inaendelea. Waziri, sijui utafanya nini ili watu wangu wapate amani. Nimeomba kila wakati kuwa hao watu watolewe maeneo ya Rugus, Mukutani na Arabal. Hao majambazi wamechukua maeneo yote matatu. Majambazi wanaishi katika shule ambazo tumejenga kutumia hela za National Government-Constituencies Development Fund (NG-CDF). Nitalalamika mara ngapi? Watu wangu hawana bunduki. Watu wangu sio kama wale wengine wenye bunduki na wanaweza kujilinda, na Waziri anaelewa. Ninaomba amani. Watu wangu wameumia na hadi sasa, sijui wamekuwa wangapi. Tufanye nini ili vita vya saa hii visimame na watu wangu warejeshewe ng’ombe waliokuwa wamechukuliwa? Serikali inisaidie na ichukue gharama ya kuzika mwili huo na kusimamia matibabu ya hao ambao wameumia. Ahsante sana."
}