GET /api/v0.1/hansard/entries/1230676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1230676,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1230676/?format=api",
"text_counter": 261,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaunti ya Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Nina swali kwa Waziri. Kwanza, nakupongeza kwa kuja Bungeni leo kutusikiza. Sisi akina mama tunazaa watoto wetu hospitalini, kisha tunapewa kile cheti cha dhibitisho. Baada ya hapo, kupata cheti cha kuzaliwa kwa mtoto inakuwa shida. Kwa nini usitufanyie wepesi? Mtoto akizaliwa, kwa nini asimaliziwe pale pale hospitalini na apewe cheti cha kuzaliwa? Tuko na shida sana upande wa Pwani kupata cheti cha kuzaliwa. Tumetengwa kwa muda mrefu. Kwa nini mtu wa Pwani ama yule wa Kaskazini Mashariki anaambiwa ni lazima alete cheti cha kuzaliwa cha babu au nyanya yake ilhali ni Mkenya? Pengine wale wazazi hawana vyeti vya kuzaliwa. Hilo limetusumbua sana Pwani. Utasaidia vipi wakaazi wa Pwani na akina mama kupata vyeti vya kuzaliwa? Asante sana."
}